Thursday, May 5, 2011

Osama Bin Laden Na Kifo Cha Bei Rahisi Kinachowafanya Wengi Wasiamini.

Osama Bin Laden

Obama akitangaza kifo cha Osama

Wananchi wakishangilia Ground Zero

Tangazo la kutafutwa kwa Osama

Osama katika gwanda za jeshi

Picha Feki ya kifo cha Osama

Eneo la tukio linalodaiwa Osama alikouliwa

kipeperushi kutoka serikali ya marekani kikielezea juu ya kutafutwa kwa Osama

Jumapili tarehe 02/05/2011 Dunia ilipatwa na mshangao pale Rais wa Marekani bwana Barrack Obama aliposimama na kuutangazia Umma na Dunia juu ya kumuua Osama Bin Laden, kiongozi wa kundi la Al Qaeda ambaye kwa miaka takriban kumi sasa alikuwa akitafutwa na marekani kwa udi na uvumba,lakini taarifa hiyo ikiwaacha watu wengi na mshangao na maswali kwa kuwa na mapungufu mengi na yanayoonekana kutokuwa na uhalisia juu ya kifo cha Jemedari huyo wa kundi la Al Qaeda aliyepata kuisumbua marekani na kuipa historia ya tukio la 9/11 na kumuongezea umaarufu zaidi ya ule aliokuwa nao mwanzo,taarifa hiyo ilipotoka si wote walioikubali na kuna sababu nyingi iliyofanya iwe hivyo.

HIZI NDIZO SABABU KUMI NA MOJA (11) ZINAZONIFANYA MIMI BINAFSI KUUNGANA NA MAMILIONI YA WATU DUNIANI KOTE WASIOAMINI JUU YA KIFO HICHO.
(1).Wapakistani kukikataa kifo hicho,Marekani ikiwa inadai Pakistani ndiko mauaji ya Osama yalikofanyika Raia wengi wa nchi hiyo wamekataa kukikubali kifo hicho kwa jinsi mazingira ya kifo yalivyoandaliwa kwani inaonyesha wazi toka mwanzo haikuwa rahisi kwa Osama kuishi nchini humo, na hata Raisi wa Pakistani alishawahi kukanusha juu ya kujificha Osama nchini kwake akieleza kuwa kwa jinsi Pakistani inavyoishi sio rahisi kwa mtu kuishi bila kufahamika na watu wengine,kwani watu wa Pakistani wanaishi kwa kufahamiana pengine kuliko hata nchi nyingine yoyote duniani.
(2).Picha ya Uongo ya kifo cha Osama,watu wengi wakiwa wanaanza kuikubali taarifa ya kifo hicho kulikuja kuzuka habari kuwa picha zilizotolewa sio za kweli kwani mazingira ya kifo,nguo zinazoonekana katika picha,sehemu ya bega na uso havikuendana hivyo hakukuwa na uhalisia wowote wa kuunganisha picha hiyo na mazingira yanayoizunguka,na baadae U.S officials walikuja kutoka tamko la kuonya kuwa picha hiyo ni feki kwa kituo cha NBC news,sasa swali ni je picha halali ya Osama akiwa amekufa ziko wapi?.
(3).Sehemu aliyozikiwa baada ya kufa,hili ni jamo lingine lililoishangaza dunia,wakati marekani inadai imeutupa ama kuuzika mwili huo baharini dunia ya werevu imekataa na mimi nikiwamo kwani tunakumbuka jinsi wamarekani walivyokuwa wakimsaka Osama na hata Kuandika wanamtaka akiwa DEAD or ALIVE hivyo hawawezi kutuambia mtu huyu waliyetumia mabilioni ya dola kumsaka baada ya kumuua wakamtupa kirahisi baharini bila kuuonyesha ulimwengu nini walichomfanya ili iwe fundisho kwa watu wa aina yake,NO hiyo haingii akilini hata chembe,na kufanya jambo liwe gumu vyombo vya habari ikiwemo Al Jazeera vimefatilia kwa karibu juu ya swala la maziko hayo na kusema bado ni utata huku akilini mwa watu wengi jibu likiwa ni UONGO MTUPU kama sio WIZI MTUPU.
(4).Kutopatikana hata tukio moja wakati wanajeshi wakivamia na kushambulia eneo alilodaiwa kuuawa Osama,Wakati Dunia inafahamu nguvu ya teknolojia ya taifa la marekani na kumekuwa na mazoea aidha ya kupata picha za moja kwa moja (live feed) ama marudio ya tukio baada ya kutokea wakati marekani ikiwanyaka maadui zake, tumeona hiyo kwa Sadam Hussein wakati anakamaywa,na magaidi kadhaa waliopatwa kukamatwa hivyo huwezi kutuambia tukio la kumkamata na kumuua gaidi huyo aliyeifanya marekani ikaingia katika kitabu cha kumbukumbu ya tukio la september eleven haikuwa muhimu kiasi hicho kuonekana duniani kwa faida ya wamarekani na dunia nzima,ina maana hakukuwa na camera au satelite eneo la tukio,au hawakupenda kumdhalilisha kama walivyomdhalilisha Sadam Husein kwa kumnyonga hadharani dunia ikishuudia Live?,kwangu hiyo nayo ni propaganda kama zilivyo fact tatu zilizotangulia,hivyo marekani bado ina kazi ya kutuelewesha zaidi.
(5).Kufa kirahisi kwa kupigwa risasi kichwani,kila mtu anafahamu what Osama Bin Laden is capable of,hivyo marekani itupe sababu ama picha kamili ya kilichotokea mpaka jamaa huyu akapigwa risasi kichwani kirahisi kiasi hicho,swali ni je kama alikamatwa kisha kupigwa risasi kwa nini hawakumsafirisha mtu huyu marekani kwani alikuwa akitakiwa DEAD or ALIVE,na kwa kuwa ni jambo la ulimwengu mzima sasa kwa nini wasitueleze jinsi tukio zima lilivyotokea,labda ni mwanajeshi yupi anahusika na kifo cha gaidi huyo ili dunia impongeze na kumpa haki yake ya ushujaa,zaidi ya kutuambia tumemuua kwa risasi ya kichwa.
(6).Eneo la tukio alilodaiwa kuuawa Osama,katika picha zinazoonyeshwa na vyombo vya habari ni picha tu ya chumba kikiwa na kitanda,nguo kadhaa na damu ikiwa imezagaa,swali ni je kuna chochote kinachothibitisha hilo ni eneo la tukio ya kifo hicho,au ni nyumba tu kama nyumba nyingine yoyote inayoweza kuwepo katika eneo lolote duniani ikiwa na kitanda,nguo na damu?,na kama tukio la kukamatwa na kuuawa lipo katika video basi lingetuonyeshwa nyumba ama chumba hicho na kutufanya tuamini kweli ni sehemu husika.
(7).Obama kukataa kutoa picha za mwili wa Osama,wakati dunia ikitafakari juu ya ukweli halisi mshangao mwingine unakuja wakati rais Obama anapokataa kutoa picha za marehemu Osama Bin Laden,aliyazungumza hayo akiongea na mwandishi Steve Kroft wa kituo cha CBS news,kisingizio ni kuwa picha hizo hazifai kuonekana hadharani,sasa swali ni je kati ya kumnyonga mtu hadharani dunia ikishuhudia na kutoa picha ya maiti iliyouawa kipi ambacho hakifai kuonekana hadharani?,tumeona jinsi gani marekani inavyoweza kuwadhalilisha adui zake sasa iweje iwe na aibu na huyu aliyeuwa maelfu ya wamarekani, wakati ilimnyonga Sadam ambaye hakuuwa hata raia mmoja wa kimarekani na hakuwa akitafutwa tuliona tukio zima licha ya haki za binadamu kupiga kelele.
(8).Ukimya wa Osama kwa miaka mingi sasa,Kuna watu wanalazimika kuamini kuwa marekani hawakumuua Osama na hajafa,na kama amekufa basi si wao wamarekani waliomuua,Osama amekuwa kimya kwa miaka mingi sasa na hata baadhi ya vyombo vya habari kuamini alishakufa,hakuonekana,kuzungumza wala kuonyesha dalili zozote za uwepo wake duniani,hivyo kuna asilimia kubwa kuwa kama ni kufa basi alikufa kwa matatizo ama maradhi mengine na si wamarekani na ndio sababu wamarekani hawana picha,video hata sauti ya tukio la mauaji yake na hawawezi kuthibitisha kifo hicho kwa vitendo.
(9).Kuuawa kirahisi baada ya kuwasumbua miaka zaidi ya kumi,tunafahamu kuwa Bill Clinton alimtafuta kimya kimya,George Bush akamtafuta kwa kelele na mbwembwe nyingi na hakufanikiwa kukamata hata nguo alizokuwa anavaa Osama,sasa leo iweje Obama ambaye hata hakuonyesha nia ya kushughulika na jamaa huyo kuibuka kidedea tena kirahisi kwa kumpiga risasi kichwani na kumtupa baharini,inaonekana basi Obama hataki makuu kwani kamuua osama kimya kimya pia hakutaka picha zozote za video zichukuliwe,na sasa hataki hata kutuonyesha picha za marehemu kwani Osama hakuwa BIG DEAL KWAKE.
(10).Kifo hicho kuhusishwa na uchaguzi mkuu ujao wa marekani,wote tunakumbuka moja kati ya vitu vilivyompa kura nyingi na kumuingiza madarakani Obama mwaka 2008 ni swala la kutaka kulifunga gereza la Guantanamo bay,na kuwarudisha wanajeshi wa marekani kutoka Iraq na Afganistani,lakini miaka imekatika na uchaguzi wa awamu ya pili umewadia Rais huyo akiwa hajatimiza ahadi zake hizo kwani Guantanamo bay bado iko na mateso yake yakiendelea kama kawaida,na wanajeshi Afganistani wakiendelea na mbilinge zao za vita hiyo ya kila siku isiyoisha,wachunguzi wa mambo wanathubutu kusema kifo hiki cha kupandikizwa ni njia ya kumuongezea umaarufu Obama na kumpa nafasi ya kuchukua tena kiti chake cha urahisi kwani kushindwa kwake kutekeleza ahadi zake zile mbili ilikuwa ni kuti kavu ambalo bila shaka lingemuangusha Obama katika Uchaguzi mkuu mwakani.
(11).Hisia ya marekani kutaka sifa kwa jambo lisilowahusu,swali ni je gaidi yeyote wamarekani wanaomtafuta hawezi kufa kwa uwezo wa mungu mpaka wao wamkamate au kumuua?,inawezekana kweli Osama amekufa lakini si wamarekani waliomuua na inawezekana alishakufa miaka mingi sana na ndo maana alikuwa kimya kwa kipindi kirefu bila kuzungumza chochote,na wamarekani inawezekana wamepata nafasi ya kugundua hilo siku za karibuni na kuamua kulitungia hoja,mwandishi Mark Pasetsky anasisitiza kuwa kuna ulazima wa picha za Osama akiwa amekufa zitolewe ili kumaliza utata wa kifo hicho na kama ni kuipa credit marekani basi tuipe kihalali na si kwa kusubiri mtu ajifie mwenyewe sifa wapate wao.
Huo ni mtazamo wangu na si hoja,pia hauhusiani na upande wowote.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...